Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mapambano yake dhidi ya vitendo vya
udhalilishaji wa Kijinsia vilivyokithiri katika maeneo mbali mbali
Nchini, kamwe haitamvumilia, kumuonea aibu, wala muhali Mtu yeyote wa
cheo chochote na ngazi yeyote pindi atakapobainika kuhusika na vitendo
hivyo.
Akitoa
Hoja ya kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi
Zanzibar uliokuwa ukifanyika katika Majengo ya Baraza hilo Chukwani Nje
kidogo ya Mji wa Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi alionya na kutahadharisha wazi kwamba Viongozi na Wananchi
wanapaswa kutambua kuwa Sheria ni Msumeno.
Balozi
Seif alisema Serikali itaendelea kuchukuwa hatua kali za kisheria dhidi
ya wote watakaobainika kushiriki katika kadhia hiyo ikiwemo wafanyaji
na wale wote wanaoshiriki katika kuwalinda na kuwakingia kifua wahalifu
wote wa masuala ya udhalilishaji wa kijinsia.
Alivinasihi
vyombo vya ulinzi na usalama kupambana zaidi dhidi ya vitendo hivyo
vinavyolitia aibu Taifa sambamba na kuharibu maisha ya Wananchi, huku
Jamii ikipaswa kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo hivyo katika
Mkakati wa kukabiliana na tatizo hilo baya Kijamii na hata Kidini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar katika Majengo ya Baraza hilo yaliopo Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya Mawaziri wa SMZ na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotuba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipotoa Hoja ya Kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar .
Baadhi ya Manaibu Mawaziri wa SMZ na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakimsikiliza Balozi Seif alipokuwa akisoma Hotuba ya Kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar M,h. Zubeir Ali Maulid akiongozwa na Askari wa Baraza hilo wakitoa nje ya Ukumbi baada kufungwa kwa Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi huko Chukwani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Jimbo la Dimani Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini baada ya kufungwa kwa Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi.Picha na – OMPR – ZNZ.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...