WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mkoa wa Mtwara kupambana na makundi ya watu yanayotaka kuharibu masoko ya korosho.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa mnunuzi aliyekataa kununua korosho kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha ubora wa korosho alichokikuta ghalani.Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Februari 28, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba.

“Tandahimba korosho zote ni daraja la kwanza sasa korosho chafu zinatoka wapi? Kuna kundi linataka kuharibu soko lazima tupambane nalo.”Waziri Mkuu ameongeza kuwa “lazima mshirikiane kuwabaini walioleta korosho chafu Tandahimba na wakipatikana wachukuliwe hatua kali za kisheria.”

Amesema haiwezekani mnunuzi amenunua korosho daraja la kwanza alafu anakuja anakuta korosho nyingine tena chafu, lazima waliozibadilisha wasakwe. Awali, Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Amama Farms, ambapo ametoa wito kwa walionunua viwanda vya korosho wafunge mashine mpya na kuanza uzalishaji.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa (kulia) wakimsikiliza Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, Abdulrahman Sinani, wakati alipotembelea kiwanda hicho, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Gasper Byakanwa, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mbanguaji korosho Zuhura Abdallah, katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, katikati ni Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Gasper, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa mashine ya kuchambua korosho na Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Abdulrahman Sinani  katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia ubora wa korosho, iliyo teyari kuliwa, wakati alipotembelea Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...