Na Jumbe Ismailly -HANANG        
PAMOJA na serikali ya awamu ya tano kutangaza elimu bila malipo kuanzia shule za msingi hadi kidato cha nne,lakini wazazi na walezi wa wanafunzi katika Halmashauri ya wilaya ya Hanang bado wamekuwa kikwazo cha watoto wao kufanya vizuri katika mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Brycosen Kibassa aliyasema hayo kwenye mahojiano maalumu na kituo hiki alipokuwa akizungumzia kushuka kwa kiwango cha elimu katika wilaya hiyo kutokana na wazazi au walezi kuwashawishi watoto wao kufanya vibaya kwenye matokeo ya mitihani yao ya kumaliza masomo yao.
Aidha Mkurugenzi huyo aliweka bayana kwamba mwaka 2017 Halmashauri hiyo iliweka mpango na wakakubaliana kwamba kiwango cha ufaulu kwa wastani uwe asilimia 80 kwa wilaya na licha ya kufanya majaribio mengi kabla ya kufikia mtihani wa taifa,ambapo katika mtihani wa majaribio walipata wastani wa asilimia 75.
Kwa mujibu wa Kibassa baada ya kufanya mtihani huo wa kitaifa wamepata asilimia sita hali ambayo ni dhahiri kwamba iliwashitua sana na kuanza kuangalia kilichosababisha hali hiyo na katika taarifa za awali walizonano inaonekana wazazi wenye mwamko mdogo wa elimu katika eneo hilo waliwatuma kwa makusudi kabisa watoto wao kwamba wahakikishe hawafanyi vizuri katika mitihani yao.
  Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,CharlES Yona akisisitiza juu ya umuhimu wa kudumisha ushirikiano katika utendaji wa shughuli zote za Halmashauri ya Hanang,lengo likiwa ni kuisogeza mbele kimaendeleo Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Bryceson Kibassa (wa kwanza kulia) akimpongeza diwani wa kata ya Nangwa,Portagia Baynet muda mfupi baada ya kuapisha na kula kiapo cha uadilifu.


 Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara wakiwa wamesimama kwa muda wa takribani dakika tano kuashiria kumkumbuka mmoja wa madiwani hao aliyepoteza maisha katika siku za hivi karibuni.
 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Nangwa waliohudhuria mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo wasikiliza kinachojadiliwa na wawakilishi wao waliowachagua.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...