MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema Machi 1 mwaka huu, itatoa uamuzi dhidi ya maelezo ya onyo yaliyotolewa Polisi na Mbunge wa Kawe Halima Mdee, (Chadema), katika kesi ya kutumia lugha ya matusi (chafu),dhidi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.John Magufuli yapokelewe kama kielelezo au la.
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa baada ya shahidi wa upande wa mashtaka D/SSGT Albogast kuomba kuyatoa maelezo hayo ya onyo mahakamani hapo kama kielelezo na Wakili wa Utetezi Peter Kibatala kupinga kwa madai yalichukuliwa nje ya muda.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama hiyo kusikiliza pande zote mbili ule wa utetezi na mashtaka na kueleza Machi Mosi, mwaka 2018 atatoa uamuzi kama maelezo hayo ya onyo yapokelewe ama yasipokelewe kama kielelezo.
Katika kesi hiyo, Mdee anadaiwa kuwa, Julai 3, mwaka 2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa Wilaya ya Kinondoni alitumia lugha ya matusi dhidi ya Rais Magufuli kuwa “anaongea hovyohovyo , anatakiwa afungwe breki” kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...