Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni mstaafu George Mkuchika amewataka wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa kufanya Kazi kwa kufuata sheria taratibu na kanuni kwa kuzingatia matakwa ya Kazi waliyoajiliwa nayo.
Aidha amewata kuwa waadilifu na kutojihusisha na masuala ya kupokea rushwa wakati wanapotimiza majukumu yao ya kazi kuepuka kuipaka matope ofisi hiyo nyeti yenye maadili,
Amesema idara hiyo ni nyeti kwa kulinda maadili ya viongozi wa umma na ni matarajio ya watanzania kuona watumishi wa taasisi hiyo hawajihusishi na vitendo vitakavyoipaka matope taasisi hiyo na serikali kwa ujumla.
Mkuchika ameyasema hayo leo katika ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa taasisi hiyo katika ziara ya siku moja.
“Nyinyi ndiyo mnaosimamia maadili ya viongozi siyo wafanyabiashara mkishawishiwa kwa vyovyote vile na kujihusisha na rushwa wakati mnapokuwa katika majukumu ya kuwakagua hawa viongozi mtakuwa mmeipaka matope taasisi na wizara kwa ujumla wake.
“Sitarajii kusikia mfanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akipandishwa mahakamani kwa kujihusisha na masuala ya rushwa atakuwa amevunja sheria na atachukuliwa hatua za kinidhamu na za kisheria kama mhalifu mwingine. Lakini kikubwa zaidi ni jambo baya kwenu lakini pia ni jambo baya kwa taasisi ya umma,"amesema.
Wakati huo huo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano huo, Mkuchika amesema, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanaruhusiwa kupanda kwenye majukwaa na kuwanadi wagombea wa CCM kwa sababu wana vyeo vya kisiasa hata kama wapo serikalini
Amesema kutokana na hali hiyo, viongozi hao wanaweza kupanda kwenye majukwaa ya kisiasa na kunadi sera za chama chao kwa wananchi ili wazijue.
Amesema RC na DC ni wateule wa Rais, lakini ni vyeo vya kisiasa ambavyo vimeanzishwa kwa ajili ya kusimamia na kutekeleza shughuli za chama na Serikali.
"Hivyo basi kupanda kwenye majukwaa na kunadi sera za mgombea wao si kosa kwa sababu ni sehemu ya kazi yao na kabla ya kuchaguliwa tayari walikuwa wanachama wa CCM," amesema.
Ameongeza, hakuna sheria inayowabana viongozi hao wasisimame kwenye majukwaa na kunadi au kueleza sera ya chama chao kwa wananchi.
Amesema watendaji wa Serikali na wakurugenzi na Katibu Tawala ambao kwa mujibu wa sheria, hawaruhusiwi kusimama kwenye majukwaa na kunadi sera za chama, kwa sababu ni mtendaji wa Serikali na yupo kwa ajili ya kuhakikisha majukumu ya Serikali yanaendelea kwenye maeneo yao.
Akizungumzia hatma ya mafao ya watumishi waliokutwa na vyeti feki na kuondolewa kazini amesema, walichokifanya watumishi hao ni kinyume na sheria, hivyo basi wasubiri huruma ya malipo ya stahiki zao kama itakuwepo.
"Serikali ilifanya kikao na Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi nchini(Tucta) ambao waliomba huruma kwa watumishi hao ili waweze kupewa chochote, kwa sasa suala hilo linafanyiwa kazi lakini bado hakuna uamuzi wowote uliotolewa kuhusu suala hilo," amefafanua.
Amesema watumishi walioghushi vyeti wasubiri huruma ya serikali ya kulipwa au kutokulipwa stahiki zao kwa sababu kosa walilolifanya ni kubwa na sheria hairuhusu kughushi vyeti.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika akizungumza na wafanyakazi.
Wafanyakazi mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika wakati alipokuwa akizungumza nao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...