Na Chalila Kibuda,Blogu ya jamii

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeandaa mkutano wa wadau kwa lengo la kuwasilisha mpango mkakati wake wa miaka mitano na kupokea maoni yao.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mjumbe wa Bodi ya VETA, Suleiman Lolila amesema mpango mkakati huo utatoa picha halisi ya mamlaka inachotarajia kufanya ndani ya miaka mitano.Lolila ametaja baadhi ya malengo hayo ni kuboresha utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi , kupanua wigo wa utoaji mafunzo ya elimu na ufundi stadi ili kufikia makundi mengi zaidi na kuimarisha menejimenti ya VETA .

Amesema malengo mengine ni kupunguza maambukizi wa virusi vya Ukimwi na kuboresha huduma saidizi na kutekeleza mpango wa taifa dhidi ya rushwa.Pia amewaomba wadau kutoa mawazo yao ili kuboresha mpango mkakati huo na Bodi hiyo itapokea mawazo hayo na kuyajumuisha katika mpango mkakati na kusimamia utekelezaji wake kwa kuweka mazingira rafiki na kutoa usimamizi wa karibu.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dk. Bwire Ndazi amesema mpango mkakakati huo umeandaliwa kwa kuzingatia hali halisi ya kiuchumi na kijamii ili kuhakikisha ajenda ya Serikali ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda.“Katika miaka mitano ijayo (2018/2019 hadi 2022/2023) mamlaka hiyo imejikita katika uboreshaji wa utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi ili kuwa na mafundi stadi mahiri na wa kutosha nchini,”amesema.

Dk.Ndazi amesema baadhi ya malengo waliojiwekea ni kuongeza udahili wa wanafunzi katika vyuo vya ufundi stadi kutoka 200,000 hadi 700,000, udahili wa watu 400 wenye mahitaji maalum kila mwaka, udahili wa vijana 2400 wanaotoka katika mazingira magumu kila mwaka.

Amesema wataongeza idadi ya udahili wa wanafunzi wa kike kutoka asilimia 35 hadi 45,utambuzi na Urasimishaji wa vijana 200,000 waliopata mafunzo kupitia mfumo usio rasmi,Ujenzi wa vyuo vipya vya VETA visivyopungua 13 nchini.

Mkutano huo umehusisha wadau mbalimbali wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi ikiwemo maofisa wa Serikali, wawakilishi kutoka mashirika ya kimataifa likiwamo Shirika la Kazi Duniani(ILO), ISTEP, IYF na VSO, wawakilishi kutoka katika viwanda, watoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi pamoja na wazazi.
 Mjumbe wa Bodi ya VETA, Suleiman Lolila akizungumza wakati wa ufunguzi wa  mkutano wa wadau wa VETA wa  kutengeneza mpango wa miaka mitano leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa VETA, Dk. Bwire Ndazi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mikakati ya miaka mitano iliyopita na mafanikio yake leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Ajira , Hildegardis Bitegera akizungumza kuhusu maendeleo ya VETA  katika suala la ajira leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wadau wa katika mkutano wa kutengeneza mkakati wa miaka mitano 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...