Na Karama Kenyunko,Globu  ya Jamii.
WATU 28, wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kukusanyika isivyo halali.
Mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa, watuhumiwa hao wote wanadaiwa kuwa Februari 16, mwaka huu huko Kinondoni katika eneo la Mkwajuni lililopo katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, walifanya mkusanyiko usio wa halali .

Mwendesha Mashtaka wakili wa Serikali, Faraji Nguka leo akisoma mashtaka amedai, lengo la mkusanyiko huo wakiwa na nia ya kufanya uvunjifu wa amani na kusababisha taharuki kwa wananchi.
Hata hivyo, washtakiwa wote wamekana kuhusika kwenye tukio hilo na baadhi yao wameweza kutimiza masharti ya dhamana ambayo yamewataka kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakaesaini bondi ya shilingi milioni moja na nusu.
 Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 8, mwaka huu.


Baadhi ya majina ya watuhumiwa hao ni, Tabitha Mkude, Haji Lukwambe, Emmanuel Kimoi, Mohammed Juma, Hussein Mnombo, Abdallah Hamisi, Hussein Kidela, Paulo Kimaro, Brayan Morris, Hussein Nguli na Edina Kimaro.
Wengine ni Fatuma Ramadhani, Asha Kileta, Salha Ngondo, Ally Rajabu, Raphael Mwaipopo, na Athumani Mkawa.

Katika mkusanyiko huo, Mwafunzi wa mwaka wa kwanza wa chuo cha NIT Aquilina Akwelini aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala, polisi bado wanaendelea na uchunguzi kujua chanzo cha kifo chake.
WATU 28, wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia Chadema (CHADEMA), wakiwa wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kukusanyika isivyo halali. Picha na Mody

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...