Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga 
 WATU 17 kati ya 26 waliofariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea Mkuranga Mkoani Pwani ,wametambuliwa majina yao ambapo hatua inayoendelea ni kuwakabidhi kwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi. Aidha watu wengine 10 waliojeruhiwa walikimbizwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa matibabu. 
 Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T.676 DGK (pichani) inayofanya safari zake Kimanzichana - Mbagala Rangi na gari nyingine aina ya Lori. 
 Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga, Stephen Mwandambo alisema amepokea maiti 25 na majeruhi hao ambapo majeruhi mmoja alifariki njiani wakati wakipelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 
 Mganga mkuu huyo aliwataja waliofariki na kutambuliwa majina yao ni 17 kati ya 26 waliofariki kuwa ni pamoja na Selemani Guli (36) mkazi wa Kongowe,Modesta Sheleli (24 ) mkazi wa Vianzi,Doreen Selemani Seleli (5), sheila Hamad Mkuba ( 8 )mkazi wa Vianzi na Mariam Hussein Sadik (15 )mkazi wa Mwarusembe. 
Wengine aliotaja ni Nassoro Hamis( 48) mkazi wa Jaribu Mpakani, Asha Athumani (24)mkazi wa Songosongo ,Nasma Athuman 22 Songosongo Mwanahawa Athuman (52),Mohammed Saidi (25) mkazi wa Njopeka na Mwajabu Jongo (20)mkazi wa Njopeka"; 

 Dokta Mwandambo aliwataja marehemu wengine kuwa ni Mwarami Mbunju(37) mkazi wa Mkamba na Abisaalom Uloga (25)mkazi wa Kimanzichana ,Kijongo Kibwana Jongo(26 )anakaa Jaribu Mpakani na Recho Japhet (16),Mariam Selemani (36)mkazi wa Mbagala na Melania Kapatwa (38)mkazi wa Jaribu Mpakani.


Kaimu kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Kibiti Mohammed Likwata akithibitisha anesena ajali imetokea usiku wa kuamkia machi 25 mwaka huu katika eneo la Kitonga kata ya Mwalusembe wilaya ya humo. 

 Chanzo cha ajali inadaiwa mwendo kasi wa dereva wa lori katika kilima na kusababisha ajali hiyo mbaya. Simanzi zimetawala katika wilaya hiyo ,ambapo mbunge wa jimbo la Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega aliishukuru serikali ya wilaya chini ya mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga kwa juhudi zake za kusaidia majeruhi na marehemu kupelekwa hospitalini. 
 Mhe. Ulega alitoa pole kwa wafiwa na majeruhi na kuwaasa madereva waache kuendesha kwa mwendo kasi kwani husababisha ajali zembe. "Naishukuru pia hospitali ya wilaya kwa juhudi zao baada ya kupokea marehemu na majeruhi kuhangaikia kuokoa maisha yao." alieleza Ulega.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...