Na Fredy Mgunda,Iringa.
KAMPUNI
ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa imempongeza Rais Dk
John Magufuli kwa namna alivyolipatia ufumbuzi suala la sukari ya viwandani ikisema
litanusuru viwanda vilivyotaka kufungwa kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo.
Katika
Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika Ikulu jijini
Dar es Salaam, Machi 19, pamoja na mambo mengine yanayohusu sukari, Rais
Magufuli alisema hakuna sababu kwa taifa kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza
sukari toka nje ya nchi wakati uwezo wa wafanyabishara kuzalisha sukari hiyo
nchini upo.
Dk
Magufuli alisema mahitaji ya sukari nchini ni tani 590,000 kwa mwaka, ambapo
tani 455,000 ni kwa ajili ya matumizi ya majumbani na tani 135,000 kwa ajili ya
viwandani.Alisema
kwasasa kuna upungufu wa tani 125,000 za sukari ya kutumia majumbani na tani
135,000 kwa ajili ya matumizi ya viwandani.
Akizungumza
na wanahabari wakati akielezea mafanikio na changamoto uzalishaji katika
viwanda hivyo, mkurugenzi wa kampuni hizo, Suhail Esmail Thakore alisema
wamepokea kwa furaha kubwa uamuzi wa serikali wa kushughulikia upungufu huo.
“Namshukuru
Mheshimiwa Rais kwa kuchukua hatua ya haraka sana kushughulikia tatizo la
sukari. Taarifa tuliyopata mara baada ya kikao kile ni kwamba taratibu za
kupata vibali vya kuagiza sukari ya viwandani kwa kuzingatia mahitaji ya
viwanda vyetu zinaendelea. Hiiimetupa uhakika wa kuendelea na uzalishaji,”alisema.
Alisema
viwanda vyake viliingiwa na hofu ya kusimamisha uzalishaji baada ya serikali
kuzuia uagizaji wa sukari hiyo toka Novemba mwaka jana.“Viwanda
vyetu vivyoatumia malighafi zinazozalishwa na wakulima wa ndani ya nchi,
zinazalisha bidhaa mbalimbali zinazojulikana kwa jina la Ivori zikiwemo tomato
na chill sauce, pipi, chocolate na unga wa cocoa,” alisema.
Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya mafanikio ya sekta ya viwanda yanavyozidi kukua na kumpongeza Rais wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuinua sekta viwanda hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...