HATIMAYE Kampuni ya Simu ya Airtel yawatendea haki wana Gairo.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Airtel.
Kwa kiasi kikubwa mtandao wa Airtel ndio mkombozi mkubwa wa wananchi wa Gairo hasa vijijini. Bado mawasiliano ya simu ni changamoto kubwa sana Gairo.Mhe. Mchembe aliendelea kuwapongeza Airtel kwa ajira zaidi ya 400 nchini kupitia ofisi zinazozinduliwa sasa. Vijana wa Gairo pia ni wafaidika wa Ofisi hizo.
Kabla ya kufunguliwa ofisi hizo, wananchi walikuwa wanaenda Dodoma au Morogoro kwa huduma mbalimbali zinazohitaji kushughulikiwa na Airtel wenyewe.Mhe. Mchembe anayakaribisha mashirika mengine ya simu kufungua ofisi Gairo. Wilaya inakuwa kwa kasi kubwa na mzunguko wa pesa ni mkubwa na mawasiliano yanahitajika kwa kasi kubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...