Na Woinde Shizza ,Arusha
WAKURUGENZI wa Kiwanda cha Grande Demam kilichopo wilayani Meru mkoani Arushawameama kuongeza thamani ya maziwa ya ng'ombe huku
wakihamasisha Watanzania kunywa maziwa yalisindikwa kwani hayana madhara kwa mlaji zaidi ya kumkinga na magonjwa yanayoweza kuambikizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
Uamuzi wa kuongeza thamani ya maziwa umetokana kiwanda hicho kuongeza wigo na kununua maziwa zaidi kwa wafugaji wilayani hapo ambao walikua wakiteseka kupata masoko na wakati mwingine kumwaga maziwa yao yanayoharibika kwa kukaa muda mrefu bila kununuliwa.
Imefahamika Wilaya ya Meru ni moja kati ya Wilaya maarufu zinazoongoza kwa uzalishaji mkubwa wa maziwa mkoani Arusha na maziwa hayo huuzwa maeneo ya miji ikiwemo viunga vya Jiji la Arusha na nje ya Jiji hilo.
Licha ya uzalishaji huo wa maziwa bado wafugaji hao wa wilaya hiyo ya Arumeru walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa masoko ya uhakika ya kununua maziwa hayo, hivyo kusababisha kuharibika baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kununuliwa.
Akizungumza leo mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda hicho Dk.Deo ambaye ni mtaalam wa mifugo anasema kutokana na changamoto hiyo kwao wakaifanya kuwa fursa ya wao kuwekeza kiwanda cha kusindika maziwa.
Dk.Deo anasema kwa kuwa wafugaji hao walikua wakiyamwaga maziwa yao yaliyokuwa yakiharibika kwa kukosa soko la uhakika na hawakuwa na namna yoyote ya kuongeza thamani maziwa hayo ili yaweze kukaa kwa muda bila kuharibika baada ya kuanzisha kiwanda hicho imesaidia kuongeza thamani ya maziwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...