NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amesema hatakuwa tayari kuona fedha za miradi ya maendeleo zinatumika vibaya huku akimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Sabasi Chambasi kuwa makini nayo.

Hatua hiyo inatokana na kuwepo kwa baadhi ya miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali kujengwa chini ya kiwango jambo ambalo linasababishwa na kutokuwa makini kwa viongozi wanaoisimamia. 

Aweso aliyasema hayo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani ambalo limegharimu kiasi cha milioni 600 linalosimamiwa mkandarasi Kisyeri Chambiri kutoka kampuni ya Wesers Limited.

Alisema mradi huo una umuhimu mkubwa sana kwa wilaya hiyo hivyo lazima watumishi wakiwemo wale ambao wanasimamia suala hilo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ili kuweza kuongeza ufanisi wakati wakitekeleza suala hilo.

“Mkandarasi huu mradi ni muhimu sana kwa Halmashauri yetu hivyo sitopenda kuona unajengwa chini ya kiwango lakini pia hakikisheni unakamilika kwa wakati kwa lengo la kufanya kazi “Alisema.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akimsikiliza kwa umakini Mkandarasi kutoka Kampuni ya Wesers Limited ambaye anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani Kisyeri Chambiri mara baada ya kulitembelea kuona namna linavyoendelea wakati wa ziara yake ambapo alihimiza likamilike kwa wakati kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akimueleza jambo Mkandarasi kutoka Kampuni ya Wesers Limited ambaye anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani Kisyeri Chambiri mara baada ya kulitembelea kuona namna linavyoendelea wakati wa ziara yake ambapo alihimiza likamilike kwa wakati.
Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Abdallah akizungumza katika ziara hiyo kulia Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Sabas Chambasi 
Sehemu ya jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani ambalo ujenzi wake unaendelea
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akikagua ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo kuweza kuona namna inavyoendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...