Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWENYEKITI wa Chama cha APPT-Maendeleo Peter Kuga Mziray amefariki dunia akiwa katika Hospitali ya Rabincia iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam.

Mwanasiasa huyo mkongwe amefariki jana saa nne asubuhi wakati akiendelewa kupatiwa matibabu ambako alilazwa hapo kwa muda wa wiki mbili kabla ya umauti kumfika.

Akizungumza na Michuzi Blog kuhusu kifo cha Mziray,Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini John Shibuda amesema baraza hilo limeshutushwa na kifo cha mwanasiasa huyo aliyekuwa mstari wa mbele kupogania maslahi ya watanzania na Taifa.

Shibuda amesema kwa mujibu wa taarifa za kaka wa marehemu Mziray ni kwamba msiba upo maeneo ya Faya nyuma ya kituo cha Mafuta ambako kuna nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa(NHC)zilizopo eneo hilo.

Amesema ameelezwa taratibu za kuupumzisha mwili wa marehemu Mziray zitafahamika baada ya mkewe ambaye yupo nchini Japan kuwasili nchini."Taarifa ambazo ninazo Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa kutoka kwa ndugu wa marehemu Mziray zinasema mkewe anaweza kuingia nchini kati ya siku mbili hizi.

" Akifika ndio watajua wanazika lini na huenda mwili ukaaga Jumamosi.Hata hivyo tutajua zaidi baada mkewe kuwasili nchini."Tumejulishwa mazishi ya marehemu Mziray yatafanyika katika kijiji cha Kihurio wilayani Same mkoani Kilimanjaro," amesema.

Akimzungumzia Mziray wakati wa uhai wake,Shibuda amesema baraza hilo na siasa za Tanzania kwa ujumla zimempoteza kiongozi muhimu ambaye mchango ulikuwa bado unahitajika."Ni pigo kubwa kuondokewa na mwanasiasa ambaye alikuwa anaipenda nchi na siku zote alisisimamia masuala yenye tija kwa nchi yetu.

" Alikuwa na masikio sikivu katika kusikiliza ushauri na kubwa zaidi siasa zilijikita katika kuunganisha Taifa.Ni mwanasiasa ambaye hakuwa anaamua mambo kishabiki bali aliamua kwa kuangalia maslahi ya nchi kwanza,"amesema Shibuda.

Amefafanua nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini ambayo anaitumikia hivi sasa aliichukua kutoka kwa Mziray baada ya kumalizima muda wake wa kuliongoza baraza hilo.

Hivyo amesema akiwa Mwenyekiti wa Baraza hilo kuna mambo mengi mazuri aliyayofanya kwa maslahi ya vyama vya siasa,"amesema.

Shibuda amesema kwa niaba ya Baraza la vyama vya siasa anatoa pole kwa familia,ndugu,jamaa,marafiki,wanasiasa wote na watanzania kwa ujumla na Mungu ailaze mahali pema popeni roho ya marehemu Mziray.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...