Na Agness Francis, Globu ya jamii
Kikosi cha AzamFc kukutana na Mtibwa sugar robo fainali ya Michuano Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Ambapo Mabingwa wa Afrika Mashariki na kati AzamFc watawakaribisha Mtibwa Sugar ya Mkoani Morogoro katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi
Akizungumza ofisini kwake leo Jijini Dar es salaam Ofisa Habari AzamFc Jaffary Maganga amesema kuwa wanasubiri tarehe ya mchezo huo ambayo Bado haijatajwa.
"Tunasubiri tu tarehe ya mchezo ili kujua mandalizi yetu yanakwenda vipi na ukizingatia kikosi ni kigumu, wana wachezaji wenye uwezo mkubwa na Mwalimu wao ni mzuri ila tutaakikisha tunalinda ushindi wa kuchezea nyumbani ikiwa kila Timu Ina presha ya kutaka kusonga mbele zaidi ukizingatia ni mashindano ya mtoano ambapo ukifungwa unatolewa kwenye Michuano hiyo"amesema Jaffary.
Maganga amemalizia kuwa mashindano hayo yenye heshima kubwa ambapo mshindi wa michuano hiyo hupata nafasi ya kwenda kushiriki mashindano ya kimataifa na kuiwakilisha Nchi.
Ofisa Habari Azam Fc, Jaffary Iddy Maganga akizungumza ofisini kwake leo Jijini Dar es salaam kuhusu mchezo wao dhidi ya Mtibwa sugar katika droo iliyochezeshwa ya robo Fainali ya mashindano ya kombe la shirikisho Azam sports federation cup (ASFC).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...