Na Benny Mwaipaja, WFM
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uchumi Mpana, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Dkt. Felipe Jaramilo katika ofisi za  Wizara ya Fedha na Mipango Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Waziri wa Fedha na Mipango aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuisaidia Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Joseph Magufuli  katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maedeleo hapa nchini.

Dkt. Mpango ameeleza kuwa uchumi wa nchi umeendelea kukua kwa kiwango cha  kati ya asilimia 6-7 kwa muda na hivyo kuiwezesha Serikali kuendelea na utoaji wa huduma za jamii na kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Dkt. Mpango ameeleza kuwa  pomaja na nia ya  kuendeleza mafanikio mazuri yaliyopatikana katika awamu za Serikali zilizopita, Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kwa dhati kujenga uchumi imara kwa kuendeleza viwanda na kuweka mazingira mazuri ya biashara ili kuvutia wawekezaji wa ndani na wale wa nje   kuja kuwekeza nchini , kujenga miundombinu  ya barabara, reli, umeme , viwanja vya ndege na kuongeza uwekezaji katika utoaji wa huduma za jamii kama vile elimu, afya na maji.
 Mkurugenzi wa Uchumi Jumla, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Felipe Jaramilo akifafanua jambo katika kikao na Waziri wa Fedha na Mipango kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza na ujumbe wa Mkurugenzi wa Uchumi jumla, Biashara na Uwekezaji (hawapo pichani), katika kikao kilichofanyika Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.  Doto James akisisitiza jambo katika kikao kati ya Waziri wa Fedha na Mipango na Mkurugenzi wa Uchumi Jumla, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Dkt. Felipe Jaramilo, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bi. Bella Bird na Mkurugenzi wa Uchumi, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Felipe Jaramilo, mara baada ya kikao kilichofanyika Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...