Na Agness Francis, Globu ya jamii

TIMU ya Azam FC imeendelea kujifua kikamilifu kwa lengo la kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Singida United, utakachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam Jumamosi wiki hii.

Mchezo huo utachezwa saa moja usiku na utakuwa na msisimko wa aina yake hasa kwa kuzingatia timu zote mbili zinakaribiana kwa ponti kwenye msimamo wa ligi.Azam FC ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 35 wakati Singida United ipo nafasi ya nne ikiwa na alama 34.

Wakati timu hizo zikiwa kwenye nafasi hizo, Simba ndio ipo kileleni kwa kuwa na pointi 45 wakati Yanga inashika nafasi ya pili.Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche na kiungo Frank Domayo wamesema kuwa wanauhakika wa ushindi kwenye mchezo huo.

Cheche amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa wachezaji wote wako vizuri na wana morali ya mchezo."Tuko vizuri tunaangalia michezo iliyopita, matatizo tuliyokuwa nayo kwenye michezo iliyopita tunajaribu kuyasawazisha yasijirudie katika mchezo ujao."Halafu tunaiangalia Singida jinsi gani ilivyo ina uzuri gani ina udhaifu gani ili tutumie madhaifu yao na mazuri yao tuweze kuyadhibiti,"amesema Cheche na kuongeza 

"Tahadhari lazima tuingie nayo kwani hatutaki kufungwa .Tunataka kushinda."Kiungo Frank Domayo amesema watapambana na kufuata maelekezo ya mwalimu ili kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Singida United.

Katika mchezo wa raundi ya kwanza, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 mchezo uliofanyika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma, bao la Azam FC ilikifungwa na Paul Peter huku Singida wakitangulia kutupia mchezaji wake Danny Sengimana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...