Na Emmanuel Masaka,Globu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatangazia wananchi wote ambao wamewasilisha malalamiko kwenye ofisi yake dhidi ya taasisi za fedha na benki kufika ofisini kwake kesho kuanzia saa mbili asubuhi.

Taarifa yake kwa vyombo vya habari ambayo ameitoa leo, Makonda amesema wananchi hao wafike kwa ajili ya kupatiwa majibu yao na kufafanua walengwa ni wale waliosikilizwa na jopo la wataalamu na wanasheria wakati wa wiki ya RC Makonda kutoa msaada wa kisheria kwa wanyonge iliyofanyika January 29 hadi February 03 mwaka huu.

.Mchakato wa kutoa majibu unaendelea ambapo leo ilikuwa ni zamu ya wananchi wenye malalamiko dhidi ya kazi na ajira pamoja na mirathi.

"Kilichofanyika leo na kitakachofanyika kesho ni mwendelezo wa kutoa majibu kwa wananchi wa Dar es Salaam ambao wamekimbilia kwa Mkuu wa Mkoa ili kupata msaada wa kisheria,"imesema sehemu ya taarifa hiyo.
RC Paul Makonda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...