Na Joel Maduka,Geita

Serikali kupitia Shirika la Viwango nchini, TBS limetakiwa kuchunguza kemikali bandia zinazouzwa na wafanyabiashara wasio waaminifu kwa wachimbaji wadogo wa madini hali inayosababisha hasara kwa wachimbaji hao.

Rais wa Shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini nchini, (FEMATA) Bw John Bina amesema hayo baada ya kikao kilichowakutanisha wachimbaji wadogo Mkoani Geita kwa lengo la kujadili namna Serikali inavyoweza kufanikisha ujenzi wa soko la madini kwa kanda ya ziwa.

Alisema baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiuza kemikali bandia kwa wachimbaji wadogo na hivyo kuwasababishia hasara.“Tunaomba serikali na TBS kuangalia sanaa haya madawa ambayo yanaingia nchini kuhakikisha wanachunguza kemikali hizi kwani kwa sasa uzalishaji unashuka kwa kiasi kikubwa wa madini ,na nyie wachimbaji niwaombe muwe mnachunguza kabla ya kununua kwani kweli mnaingia hasara kubwa sanaa”Alisisitiza Bina.

Mmoja wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Bw Nuru Shabani alisema kwa kuuziwa Kemikali hizo bandia amekuwa akiathirika katika shughuli zake.“Kiukweli tunaathirika sanaa na hili halina ubisha sasa hivi unaweza kununua tani moja ya kaboni unakuta inapitisha bila ya kushika mali inamaana hadi iwe na pipim kuanzia mia saba hadi mia nane ,Ila kwa sasa nashukuru walau serikali imetambua mchango wetu na imetuthamini mimi nilikuwa naomba kupitia Kitengo chetu tuwe na wasimamizi ambao watatusaidia kubaini kemikali hizi”Alisema Nuru.

Bw John Bina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia kero za wachimbaji wadogo alisema pamoja na matatizo hayo lakini wachimbaji hao wamekubaliana kuanzishwa kwa soko la madini Mkoani Mwanza ili kudhibiti vitendo vya utoroshwaji wa madini.
Rais wa Shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini nchini, (FEMATA) Bw John Bina ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia kero za wachimbaji wadogo akizungumza na wachimbaji wadogo wakati wa kikao cha kujadili soko la madini ya dhahabu kilichofanyika Mkoani Geita .
Katibu msaidizi wa Kamati ya kushughulikia kero za wachimbaji wadogo,Bw Gregory Kibusi akijitambulisha na kuelezea lengo ambalo limewapeleka Mkoani Geita mbele ya Afisa madini wa Mkoa huo. 
Afisa madini Mkoa wa Geita,Mhandisi Ally Maganga akizungumza na Kamati ya kushughulikia kero za wachimbaji wadogo ambao walikuwa wamewasili kwenye ofisi za madini Mkoani Humo. 
Bw,Nuru Shabani ambaye ni mchimbaji mdogo akionesha kemikali ambayo amekuwa akiitumia kukamatia madini kwenye eneo la mgodi wake. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita ambaye pia ni mchimbaji ,Bw Leornad Kiganga Bugomola akiwakaribisha wajumbe kwenye mkutano wa wadau wa madini. 
Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale ambaye pia ni mchimbaji na Mjumbe kwenye kamati hiyo,Hussen Nassoro Kasu akiwataka wachimbaji kuendelea kuwa wamoja na kushirikiana kwenye shughuli zao. 
Baadhi ya wachimbaji wadogo wakiwa kwenye kikao hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...