Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Ashanti Kijaji amesema kuwa mamlaka ya
Masoko na Mitaji ni injini katika maendeleo ya uchumi hivyo ni lazima
mamlaka hiyo iwafikie wateja.
Kijaji
aliyasema hayo wakati akitunuku vyeti kwa wahitimu wa mamlaka hiyo
waliopata kwa kushirikiana na chuo cha Uingereza CISI katika fani ya
masoko na mitaji, amesema kuwa watu hawana uelewa juu ya masoko na
mitaji hivyo wanatakiwa kufikia wateja katika kutimiza adhima ya
serikali ya awamu ya tano yenye Kauli mbiu ya nchi ya viwanda.
Amesema
Mamlaka kwa kutumia watalaam hao lazima wafanye kazi katika kujenga
nchi na kutoa elimu kuhusiana na masoko na mitaji.Amesema kuwa kampuni
zipo nyingi lakini hazijaweza kuingia katika soko la hisa ni kutokana
na kampuni hizo kushindwa kufikiwa ikiwa ni pamoja na kupata elimu.
Naibu
Waziri huyo amesema kuwa katika kufanya kazi mamlaka hiyo lazima iweke
mpango mkakati katika kuhamasisha kampuni ziingie katika soko la
hisa.Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Dk.John Mduma amesema kuwa
wanaendelea katika kutoa huduma ikiwa ni pamoja kufanyia kazi maagizo ya
Naibu Waziri katika kuwafikia wateja na kuleta matokeo chaya ya
maendeleo ya uchumi.
Dk.
Mduma amesema kuwa katika kuwa sasa watafungua dirisha la uhamasishaji
katika kufikia kampuni ziweze kuingia katika soko la hisa.
Afisa
Mtendaji Mkuu , Nicodemus Mkama amesema mkataba wa huduma kwa wateja
waliouzindua watawafikia wateja wote kuingia dhamana ya masoko na mitaji
katika kuendrleza miradi mbalimbali nchini.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi katika uzinduzi w akitabu cha huduma kwa wateja.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji, akizindua kitabu cha Msaada wa huduma kwa wateja
Mwenyekiti wa TSEBA,George Fumbuka akitoa neno la Shukrani kwa waziri mara baada ya kumaliza kuzinduliwa kwa kitabu cha Mkataba wa huduma kwa wateja.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji, akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa wahitimu wa kozi ya ushiriki katika Masoko
Baadhi ya Wadau walioshiriki katika uzinduzi wa kitabu cha huduma kwa wateja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...