Gavana wa mji wa imo nchini Nigeria, Rochas Okorocha, akimpongeza mwanafunzi wa darasa la Sita, Anati Mujib wa Shule ya Msingi Makumbusho, anayefanya vizuri katika masomo yake darasani, wakati Gavana huyo alipoitembelea shule hiyo akiambatana na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust Fund na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, Tulia Ackson, (kushoto) kwa ajili ya kuzungumza na kuchagua baadhi ya wanafunzi Yatima na waishio katika mazingira magumu ili kuwasomesha katika shule na Chuo chake kilichopo nchini Nigeria. Gavana huyo akiwa shuleni hapo alitoa zawadi ya Dola 100 kwa kila mwanafunzi aliyeongoza kimasomo katika darasa la tano, Sita na Saba kwa kila mmoja, na Dola 200 kwa mwanafunzi wa Kidato cha tatu Shule ya Sekondari Makumbusho, Raymond Kalistus, anayefanya vizuri kimasomo darasani, ambapo pia alitangaza kumdhamini mwanafunzi huyo wa Darasa la saba, Abdul Ausi kwa kumsomesha Sekondari hadi Chuo Kikuu kuanzia sasa kutokana na kufiwa na wazazi wote wawili. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Gavana akimkabidhi zawadi ya Dola 100 mwanafunzi, Anati Mujibu

Gavana akikumbatiana kwa furaha na mwanafunzi, Abdul Ausi wa daeasa la saba aliyetangaza kumsomesha kuanzia Sekondari hadi Chuo Kikuu, kwa kuchagua nchi yeyote aipendayo kwenda kupata elimu.
Gavana akisalimiana na baadhi ya wanafunzi Yatima na waishio katika mazingira magumu wanaosoma katika shule hiyo.
Gavana akisalimiana na wanafunzi wa shule hiyo wakati akiaga kuondoka shuleni hapo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust Fund na Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson, akitoa hotuba yake na kushukuru ugeni huo.
Wakielekezana jambo. Kulia ni Tijan Babangida aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Nigeria, ambaye kwa sasa ni msaidizi wa Gavana huyo..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...