Na mwandishi wetu - WAMJJW, Dodoma
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya jamii) imeendesha Mafunzo ya siku mbili kwa ajili ya kuimarisha utendaji na kuboresha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi, weledi na uadilifu katika Wizara hiyo.
Mafunzo hayo siku mbili yanaliyofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma yamejumuisha wajumbe wa Menejimenti, Kamati ya Ukaguzi na Wakaguzi wa Ndani ya Wizara hiyo. Wawezeshaji wa Mafunzo hayo ni Bwa. Alphonce Muro na Bw. Athanas Pius kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, katika Ofisi ya Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani.
Washiriki wa mafunzo hayo wamesisitizwa kuzingatia utatu (Menejimenti, Kamati ya Ukaguzi na Wakaguzi wa ndani) katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuhakiki, kusimamia na kudhibiti utendaji mahali pa kazi ili kuongeza thamani ya huduma na kazi za kila upande katika kufanikisha malengo ya Wizara. Akitoa mada kwa washiriki wa mafunzo hayo mwezeshaji alisema,
“Uhusiano na mawasiliano kati ya watendaji hao ni muhimu katika kufanikisha maelengo ya Wizara”.. amesema Bw. A. Muro
Imeelezwa kuwa kila upande una wajibu wa msingi katika kuchangia kufikiwa kwa malengo ya Wizara, washiriki wamesisitizwa kuwa na mawasilino na kushirikiana katika kupokea na kutekeleza ushauri wa kitaalam unaotolewa na maafisa wa kitengo cha Ugaguzi na Kamati ya Ukaguzi wa Ndani kwa lengo la kuboresha utendaji na usimamizi.
Mwezeshaji
wa Mafunzo ya uimarishaji na uboreshaji wa utendaji kazi mahali pa kazi
kutoka Wizara ya Fedha na Mipango- Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa
Serikali Bw. Alphonce Muro (aliyesimama) akitoa mada kwa wajumbe wa
Menjimenti, Kamati ya Ukaguzi na Maafisa wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
kutoka Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto
(Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) wakati wa mafunzo ya siku mbili
yaliyofanyika katika Chuo cha Mipango Dodoma.
Baadhi
ya washiriki wa Mafunzo Mkakati ya kuimarisha na kuboresha wa utendaji
kazi mahali pa kazi katika Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) wakifuatilia mada ya
majukumu ya Kamti ya Ukaguzi mahali pa akzi kutoka kwa mmoja wa
wawezeshaji wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika katika Chuo
cha Mipango Dodoma.
Kaimu
katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Bw. Marece Katemba (katikati) akifuatilia kwa makini mafunzo
ya uimarishaji na uboreshaji wa utendaji kazi mahali pa kazi, wengine
Bi. Georgina Edmundi Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Wizara (kushoto)
na Bi. Josephina Rusatila Mjumbe wa Kamati (kulia) wakati wa mafunzo ya
siku mbili yaliyofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.
Mwezeshaji
wa Mafunzo ya uimarishaji na uboreshaji wa utendaji kazi mahali pa kazi
kutoka Wizara ya Fedha na Mipango- Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa
Serikali Bw. Athanas Pius (aliyesimama) akitoa mada kwa wajumbe wa
Menjimenti, Kamati ya Ukaguzi na Maafisa wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
kutoka Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto
(Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) wakati wa mafunzo ya siku mbili
yaliyofanyika katika Chuo cha Mipango Dodoma.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...