Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dr, Rashid Mfaume (wa tatu kushoto) akifungua shughuli za uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno kwa watoto waliopo katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu Buhangija, Mkoani Shinyanga katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani, Ambapo Kitaifa yatafanyika Machi 20, 2018,Tarime Mkoani Mara . Kuanzia kushoto ni Kiongozi wa msafara huo ambaye pia ni Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dr. Arnold Mtenga, Mwalimu msaidizi wa kituo hicho, Mohamed Makana na kushoto kwa mgeni rasmi ni Daktari wa Meno Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya. (Picha na Khamis Mussa )
Mlezi Jackson Leonard (kushoto) na Mlezi Flora Kankutebe wakifatilia jambo wakati watoto hao walipokuwa wakifanyiwa uchunguzi huku watoto wendine wakiwa katika msitari wakisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Mwalimu msaidizi wa kituo hicho, Mohamed Makana akiwakaribisha wageni na kutoa utangulizi wa kituo hicho
Dakt. Bingwa wa Magonjwa ya Kinywa na Meno kwa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dr, Conrad Mselle akionyesha kwa mfano namna nzuri ya upigaji mswaki kwa Zephania Bahebe mmoja kati ya watoto wanaoishi katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu Buhangija, Mkoani Shinyanga katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani, Ambapo Kitaifa yatafanyika Machi 20, 2018,Tarime Mkoani Mara.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...