Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, leo (Alhamisi) amekutana na kuwa na mazungumzo na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Gambia Mhe. Hassan Bubacar Jallow.
Jaji Mkuu wa Gambia, yupo hapa nchini kwa ziara ya kikazi ya kujifunza na kujipatia uzoefu kuhusu mfumo wa utoaji haki hapa nchini pamoja na maboresho mbalimbali yakiwamo ya maslahi ya watumishi yanayoendelea katika Mahakama ya Tanzania na Taasisi nyingine za Sheria na utoaji haki.
Jaji Mkuu Jallow amemueleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi kwamba, Gambia, baada ya mabadiliko ya Serikali yaliyofanyika mwaka jana nchini humo, ipo katika mchakato wa kuifanyia mabadiliko na maboresho sekta ya sheria nchini humo.
"Nimekuja kwa ziara ya kikazi kwa madhumuni ya kujifunza kutoka Tanzania namna gani na sisi (Gambia) tutakavyoweza kuboresha na kuifanyia mageuzi makubwa sekta yetu ya Sheria na mfumo mzima wa utoaji wa haki".
Akabainisha kwamba, anafahamu, namna gani Mahakama ya Tanzania imeweza, kwa kushirikiana na Serikali na Wadau wa Maendeleleo hususani Benki ya Dunia kufanya mageuzi na maboresha makubwa katika mfumo wa utoaji haki.
Mwanasheria Mkuu Dk. Adelardus Kilangi akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe Wilbroad Slaa walipokutana nje ya Jengo ambalo lina Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki . Mwanasheria Mkuu alikuwa akimsubiri kumpokea mgeni wake Jaji Mkuu wa Gambia Mhe. Hassan Jallow ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali akimlaki Mgeni wake Jaji Mkuu wa Gambia Mhe. Hassan Bubacar Jallow mara alipowasili kwa mazungumzo. Jaji Mkuu Jallow alisoma sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1970-1973) na pia amewahi kuwa Mwendesha Mashtaka wa iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda
( ICTR) (2003-2015).
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi akibadilishana mawazo na Jaji Mkuu wa Gambia Mhe. Hassan Bubacar Jallow, leo Ofisi kwa Mwanasheria Mkuu. Jaji Mkuu yupo hapa nchini kwa ziara ya kikazi yenye madhumuni ya kujifunza uboreshaji wa sekta ya sheria na utoaji haki hapa nchini. Baadhi ya mambo waliyobadilishana mawazo ni pamoja na uwezeshwaji kwa wanasheria wa Serikali na watumishi wengine katika sekta ya sheria kimaslahi na kimafunzo.
Habari kamili BOFYA HAPA
Habari kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...