Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
Kesi dhidi ya Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai anayedaiwa kuwa na utajiri wa kutisha kwa kumiliki mali zenye thamani ya Sh. 3 bilioni ambazo haziendani na kipato chake kuanza kusikilizwa mapema mwezi ujao.
Hayo yameelezwa leo Machi 20, 2018 na wakili wa serikali kutoka Takukuru, Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
"Mheshimiwa kesi hii leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi umekamilika, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuja kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH).
Kufuatia taarifa hiyo, hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 10, mwaka huu. Kwa ajili ya washtakiwa kusomewa Maelezo ya awali.
Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera
Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.
Gugai na wenzake wanasota mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...