NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka Wakurugenzi Watendaji wote kuhakikisha watoto yatima ambao hawana ndugu maeneo wanawasidia kupata fursa ya elimu na huduma nyingine zitakawasaidia kujiendeleza.
Mwanri alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati wa mkutano wa wadau wa elimu uliokuwa ukijadiliana juu ya kuboresha elimu mkoani humo.
Alisema Wakurugenzi Watendaji wanapaswa kusimamia kama wazazi wa watoto yatima ili wawezeshe kupata elimu kama walivyo watoto wengine ili hatimaye waweze kushiriki katika ujenzi wa Taifa katika nafasi mbalimbali.
Mwanri alisema kuwa pamoja na majukumu mengine waliyonayo Wakurugenzi Watendaji wanapaswa kushirikiana na jamii katika kuhakikisha wanawasaidia watoto kufikia malengo yao ya kupata elimu kama njia ya kwanza ya kumsaidia.
“Wakurugenzi Watendaji ndio baba na mama wa watoto yatima ni lazima muwasimamie na kuwaendeleza na njia pekee ya kuwasomesha watoto hao …miongoni mwao tutapata Madakitari , Wakuu Mikoa na viongozi mbalimbali” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Aliongeza kutowasaidia watoto hao unaweza kukuta unaacha kundi muhimu katika ujenzi wa Taifa.Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema Tabora inatakiwa kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika elimu ili iweze kupata maendeleo ya kasi na kubadilisha maisha ya wananchi wake.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora amewaomba viongozi mbalimbali wa dini na Wakuu wa Wilaya kusaidia kupambana na mimba za utotoni na zile zinazokatisha ndoto za baadhi ya wasichana kufikia malengo yao.Alisema ni vema viongozi hao wa kiroho wakatumia nafasi waliyonayo katika jamii kuelimisha jamii ili waachie watoto wa kike wasome.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua jana mjini hapa kongamano la wadau wa maendeleo ya elimu mkoani humo. Lengo la kongamano hilo ilikuwa ni kujadiliano juu ya vikwazo vinakwamisha sekta hiyo kwa ajili ya kuvitafutia ufumbuzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora Hassan Wakasubi akitoa maoni yake jana kwenye kongamano la wadau wa maendeleo ya elimu mkoani humo. Lengo la kongamano hilo ilikuwa ni kujadiliano juu ya vikwazo vinakwamisha sekta hiyo kwa ajili ya kuvitafutia ufumbuzi. Picha na Tiganya Vincent
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...