Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu
amekutana na ugeni kutoka nchini Uturuki ukiongozwa na Balozi wao Dkt.
Ali Daoutoglu mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es
salaam.
Ugeni huo umejadili namna ya kuboresha Sekta ya Afya nchini hususani katika kuboresha huduma za dharura, uzalishaji wa dawa na ubadilishanaji uzoefu wa Wataalamu wa Afya kati ya nchi hizo mbili.
Balozi Ali Daoutoglu ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tazania na ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kuimarisha Sekta ya Afya nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...