Na Mathias Canal, Geita
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli tangu ianze utendaji wake imejipambanua wazi kuwa rasilimali zote za nchi ikiwemo madini ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa hivyo ni Mali ya watanzania wenyewe sio wawekezaji wa kigeni.

Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusisitiza kuwa katika rasilimali Madini Taifa halipaswi kukurupuka kuyachimba kwa kuwa uwezo wa kitaaluma na kiteknolojia kuwezesha kuyachimba na kuyafaidi kama Taifa ulikuwa mdogo kwa mantiki hiyo, Baba wa Taifa akaenda mbali zaidi kwa kuagiza madini yasichimbwe hadi hapo Taifa litakapokuwa na uwezo wa kuyachimba ili watanzania waweze kunufaika ipasavyo.

Hayo yamebainishwa na Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko Leo 6 Machi 2018 wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Nyang'wale iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hivyo Mhe Hamim Gwiyama akiwa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita.

Mhe Biteko alisema kuwa Mwalimu kwa wakati huo alijua fika kuwa Tanzani a ikifungua milango ya kuchimba madini bila Taifa  kujenga uwezo imara wa kufanikisha lengo hilo ipasavyo, wataalamu na wafanyabiashara au wale wanaoitwa wawekezaji kutoka nje, ilimradi wanazo fedha nyingi; watalilalia Taifa na kuwadanganya watanzania na hatimaye kuweza kufaidika zaidi kutokana na rasilimali madini.
Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Nyang'wale iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hivyo Mhe Hamim Gwiyama akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisalimiana na baadhi ya watendaji katika Wilaya ya Nyang'wale mara baada ya kuzuru wilayani Nang'wale akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018.
Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Nyang'wale iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hivyo Mhe Hamim Gwiyama ikimsikiliza kwa makini Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018.
Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (aliyesimama) akielezea mikakati ya wizara hiyo wakati alipozuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018, Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nyang'wale Mhe Hussein Nassor Amari Kasu, na Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale Mhe Hamim Gwiyama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...