Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepokea tani 120 za saruji ambazo ni sawa na mifuko 2,400 ya saruji kutoka kwa Vyama vya ushirika 27 vya Mkoa huo vilivyoguswa na kempeni ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam.
Mifuko hiyo 2,400 ina uwezo wa kufyatua tofali 70,000 ambazo zitejenga ofisi 14 za kisasa kwa ajili ya Walimu.
Akizungumza baada ya kupokea mifuko hiyo Makonda amesema shughuli ya ujenzi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri na amewashukuru wadau wote wanaoendelea kuchangia kampeni hiyo inayolenga kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Dar es salaam Tumaini Wilfred amesema wameguswa na jitiada zinazofanywa na Makonda katika kuboresha mazingira ya walimu.
Amesema ndio maana wameona umuhimu wa wao kama ushirika wasibaki nyuma katika kufanikisha jambo hilo ambalo ni jema na na la ukombozi wa fikra na kuongeza ushirika utaendelea kuunga mkono kwa kila hali juhudi zinazifanywa na Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda wakwanza kulia akizungumza machache leo jijini mara baada ya upoea kupokea tani 120 za saruji ambazo ni sawa na mifuko 2,400 ya saruji leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wakiwasiri
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akipokea tani 120 za saruji ambazo ni sawa na mifuko 2,400 ya saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Dar es salaam Tumaini Wilfred leo jijini Dar es Salaam.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...