Kampuni inayoongoza kwa huduma za fedha kwa njia ya mtandao, Tigo Tanzania kupitia huduma yake ya Tigo Pesa leo imewazawadia wakala wake mamilioni ya pesa kwa utendaji wao mzuri.
Wakala RBB RBB ya Sinza, Dar es Salaam ilijishindia TZS 10 millioni kutoka Tigo Pesa, huku Said Khatib wa Mkunazini, Zanzibar akijinyakulia zawadi ya pili ya TZS 5 millioni katika promosheni iliyohusisha mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo. ‘Nilishinda zawadi ya kanda katika promosheni iliyofanyika mwezi Desemba kwa hiyo nafurahi kuwa uwekezaji na juhudi nilizofanya katika kipindi hiki vimeniwezesha kutangazwa kama mojawapo wa washindi wa kitaifa,’ Khatib alisema.
Pamoja na zawadi hizio kwa washindi wa kitaifa, Tigo pia ilitoa zawadi nane za TSH 3 millioni na TZS 2 millioni kwa mawakala bora kutoka kila kanda nchini. Pia zawadi za bonasi zilitolewa kwa mawakala wote waliofikia malengo waliowekewa katika kipindi cha promosheni hiyo.
Mojelwa Mlinga wa Ukonga, Dar es Salaam aliyeibuka kama wakala bora wa kanda ya Pwani na kujinyakulia kitita cha TZS 3 milioni alisema kuwa atatumia hela alizoshinda kuboresha mtaji wake wa biashara. ‘Nilishinda zawadi ya pili kitaifa katika promosheni iliyofanyika mwezi Desemba na nilikuwa natarajia kushinda zawadi ya kwanza kitaifa, ila nashukuru kuwa nimefanikiwa kupata zawadi ya kanda,’ alisema.
Robert
Butambele (kulia), ambaye ni Wakala wa Tigo Pesa katika eneo la Sinza,
Dar es salaam akipokea mfano wa hundi ya TSH milioni kumi kutoka kwa
Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo - Hussein Sayed (wa tatu kulia).
Butembele aliibuka mshindi wa kitaifa katika promosheni ya mawakala wa
Tigo Pesa ambapo Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake
zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo. Wengine
katika picha ni Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa - Restituta Kedmond (wa
pili kulia), Meneja wa Maendeleo ya Masoko wa Tigo - Innocent Mosha
(wa pili kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Mifumo ya Usambazaji,
Katherine Lusenge.
Said
Khatib (kulia), ambaye ni Wakala wa Tigo Pesa katika eneo la Mkunazini,
Zanzibar akipokea mfano wa hundi ya TSH milioni tano kutoka kwa Afisa
Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo - Hussein Sayed (wa tatu kulia).
Khatib aliibuka mshindi wa pili kitaifa katika promosheni ya mawakala wa
Tigo Pesa ambapo Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake
zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo. Wengine
katika picha ni Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa - Restituta Kedmond (wa
pili kulia), Meneja wa Maendeleo ya Masoko wa Tigo - Innocent Mosha
(wa pili kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Mifumo ya Usambazaji,
Katherine Lusenge.
Baadhi
ya mawakala mbali mbali walioshinda zawadi katika promosheni ya
mawakala wa Tigo pesa iliyoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Tigo
wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo. Hii ilikuwa baada
ya kupokea zawadi zao katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za
Tigo, jijini Dar es Salaam leo. Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa
mawakala wake zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni
hiyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...