Na Zainabu Nyamka, Globu ya Jamii
MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Simba, Arthur Mambeta amefariki dunia jana Alhamisi baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani kwa muda mrefu.
Mambeta aliyeanza kukipiga katika kikosi cha wanamsimbazi Simba SC mwaka 1960 ikiwa inaitwa Sunderland akicheza nafasi kiungo mshambuliaji hodari kuanzia katika klabu yake hadi timu ya Taifa.
Katika historia ya Arthur, aliyewahi kocha wa Tanzania miaka hiyo, Milan Celebic raia wa Yugoslavia alikaririwa akisema kuunda timu ya taifa bila ya Arthur Mambeta ni sawa na kula chakula bila ya chumvi au chai iliyokosa sukari.
Arthur Mambeta ndiye mchezaji pekee wa Tanzania aliyekuwemo Katika kiķosi cha kwanza cha kombaini ya Afrika Mashariki iliyocheza na West Bromwich Albion ya England mwaka 1974 Uwanja wa Nakivubo mjini Kampala, Uganda.
Katika mechi hiyo ilijumuisha wachezaji wa timu ya mbalimbali kutoka Afrika Mashariki akiwamo na mchezaji mwingine wa Tanzania aliyeteuliwa, Kitwana Manara alikuwa bechi kama kipa wa akiba kabla ya kuhamia kwenye ushambuliaji ambako pia alikuwa tishio hadi anastaafu soka.
Baada ya kustaafu soka, Mambeta alindelea kujihusisha na mchezo katika utawala na amewahi kuteuliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi Simba SC.
Hata hivyo, Mambeta alianza kujitoa taratibu kwenye soka baada ya kuanza kusumbuliwa na maradhi ya saratani yaliyosababisha akatwe miguu yake yote miwili.
Taarifa zaidi kuhusu msiba huo na taratibu zake zinataolewa kutolewa na familia ya marehemu Alhamisi.
Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Arthur Mambeta. Amin.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...