Na. Jumbe Ismailly
KUTOKANA na hali ya uharibifu wa misitu katika wilaya ya Hanang kuwa kubwa sana,Mkuu wa wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara, Sara Msafiri ameziagiza kamati za maendeleo za kata kujenga utamaduni wa kujadili katika vikao vyao juu ya hali ya uhifadhi wa misitu katika maeneo yao.
Akitoa agizo hilo kwenye mkutano wa kawaida wa Baraza la kawaida la madiwani wa Halmashauri hiyo, Mkuu wa wilaya huyo aliyataja baadhi ya maeneo ya vijiji vya Lalaji. Balangida na maeneo mengine hali ya mazingira ni mbaya sana.
“Kwa hiyo niwaombe kwamba kamati za maendeleo za kata mjadili na hali ya hifadhi ya misitu na ninazo taarifa za kutosha na nimejirisha wapo viongozi wengine ni wa kisiasa wanashiriki katika biashara ya kukata miti, kuchoma na kuuza mkaa.”alisisitiza Mkuu huyo wa wilaya.
Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya kupitia serikali kuu wameshatoa maagizo kwa watendaji kwamba mtu yeyote tule atakayetaka kukata miti hata kama aliupanda mwenyewe ni lazima apate kibali kutoka kwa Mkuu wa wilaya.
Hata hivyo Sara alisisitiza kwamba ni ukweli usiopingika na alioufanyia uchunguzi wa kina na kujiridhisha kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa,wakiwemo madiwani,wenyeviti wa vijiji,vitongoji na watendaji wanajihusisha na biashara ya kukata micti kuchoma mkaa na kuuza mazao hayo.
Mkuu wa wilaya ya Hanang,Sara Msafiri akisisitiza jambo kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Mbunge wa jimbo la Hanang,Mkoani Manyara,Dk.Mary Nagu (katikati) akipitia taarifa ya utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu iliyowasilishwa kwenye mkutano huo na kisha kutaka kufahami shilingi milioni 300 zilizoagizwa kwenye mkutano wa LAC Dodoma zitalipwa lini ili vikundi vya wanawake,vijana na walemavu viweze kunufaika na kujiongezea mitaji yao.
Katibu wa CCM Wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara, Teddy Athumani (wa kwanza kushoto) akipitia makabrasha ya mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang kujiridhisha namna watendaji wa Halmashauri wanavyotekeleza ilani ya chama tawala.
Katibu wa vikao vya Halmashauri ya wilaya ya Hanang, Stevine Yonah(kushoto) akinukuu maazimio yote ya mkutano wa Baraza hilo ili watendaji waweze kutekeleza kikamilifu maazimio hayo. (Picha zote Na Jumbe Ismailly)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...