Na Kijakazi Abdalla, Maelezo
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza bei mpya ya mafuta ambayo itaanza kutumika kesho Jumanne 13/03/2018. Akizungumza na Waandishi wa habari Afisa Uhusiano wa  Mamlaka hiyo Hassan Juma Amuor amesema kuwa  ZURA  imetangaza bei  mpya kwa kuzingatia mambo yafuatayo.
Alisema kuwa wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta duniani,thamani ya shilingi ,gharama za usafiri ,kodi za Serikali pamoja na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja. Aidha alisema kuwa bei hizo Petroli kwa mwezi wa Machi 2018 imepanda kwa shilingi moja(1)kwa lita kutoka shilingi 2,256 hadi kuwa shilingi 2,257 sawa na ongezeko la asilimia 0.04%.
Bei ya mafuta ya Dizeli kwa mwezi wa Machi .2018 imepanda kwa shilingi(68)kwa lita kutoka shilingi 2,175 hadi kuwa shilingi 2,243 sawa na asilimia 3%.
Pia Afisa Uhusiano huyo alisema  bei ya Mafuta ya taa kwa mwezi wa Machi.2018 imepanda kwa shilingi (5) kwa lita kutoka shilingi 1,641 hadi shilingi 1,646 sawa na ongezeko la asilimia 0.3%. Vilevile alisema kuwa bei ya mafuta ya Banka kwa mwezi wa Machi 2018 imepanda kwa shilingi (68) kwa lita kutoka shilingi 2,017 hadi shilingi 2,085 sawa na ongezeko la asilimia 3%.
Hata hivyo alisema kuwa bei ya Mafuta ya Ndege (Jet A-1) kwa mwezi wa Machi 2018 imeshuka kwa shilingi 4.46 kwa lita kutoka shilingi 1,811.80 hadi shilingi 1,807.34 sawa na upungufu wa asilimia 0.24%.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Hassan Juma Amuor akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mabadiliko ya bei za mafuta. Picha na Kijakazi Abdalla Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...