Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
Seleman Jafo,ameipongeza kampuni ya Coca-Cola kwa kuwekeza kudhamini
mashindano ya Shule za Sekondari nchini ya UMISSETA kwa kipindi kingine
mwaka huu na kuahidi kuwa serikali nayo pia itaendelea kuiunga mkono.
Akifungua
semina elekezi ya maofisa wa michezo kutoka mikoa 26 ya hapa nchini
iliyofanyika mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki,ambapo pia aliambatana na
Naibu Waziri wake, Joseph Kakunda, Waziri Jafo, alisema serikali
inatambua mchango mkubwa wa kampuni ya Coca-cola wa kukuza vipaji vya
michezo kwa vijana.
“Nimevutiwa sana na maandalizi na usimamizi wa mashindano ya michezo ya
UMMISETA ulivyokuwa mwaka jana,kwa hili nawashukuru Coca-Cola,nafahamu
kuwa mkataba wao ulikuwa wa kudhamini mashindano haya kuanzia mwaka 2015
hadi 2018,natoa wito kwao kuangalia uwezekano wa kuongeza muda wa
udhamini ikibidi hata kuwa na haki ya kuyasimamia moja kwa moja,”alisema
Jafo. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina elekezi ya maofisa michezo ilifanyika katika Chuo Cha Mipango cha Dodoma. Semina hiyo ilihudhuriwa na maofisa michezo wa mikoa kutoka mikoa 26 ikiwemo na Zanzibar.
Baadhi ya maofisa michezo walioshiriki semina elekezi wakifuatilia hotoba ya Waziri Jafo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo, (Kushoto) akisalimiana na Meneja wa Chapa ya Cola-Cola nchini, Sialouise Shayo. Wengine pichani ni Maofisa wa Coca-Cola na Maofisa Michezo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...