SERIKALI imepeleka sh. bilioni 1.92 katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba wilayani Mtwara kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya.

Hayo yalibainika jana (Jumatano, Februari 28, 2018) wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipozungumza na wakazi wa Halmashauri hiyo, wakati wa ziara yake.Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi alisema fedha hizo zilitolewa na Serikali ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Alisema jumla ya sh. bilioni 1.2 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha kwenye Kata ya Njengwa, ambapo aliwasisitiza watendaji kutobadilisha matumizi.Waziri Mkuu alisema ujenzi huo utahusisha chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, jengo la mama na mtoto na wodi ya wanawake na wanaume, eneo la kuchomea taka na chumba cha kuhifhadhia maiti.

“Serikali imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi yao.”Aidha, Waziri Mkuu aliwataka wananchi hao kuendelea kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.

Pia Waziri Mkuu alisema Serikali inatarajia kuipitia upya sheria ya elimu pamoja na sheria ya mtoto ili kuweka masharti ya kumlinda mtoto wa kike hususani kudhibiti mimba kwa wanafunzi.Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Gelasius Byakanwa alisema Serikali itawachukulia hatua watu wote watakaobainika kuwapa watoto wa kike dawa za uzazi wa mpango ili kuwazuia wasipate mimba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...