Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara mzunguko wa 19 inaendelea kesho kwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Simba ya Dar es Salaam dhidi ya Stand United ya Shinyanga
Mchezo huo utakaochezwa saa 10 jioni utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa.
Mwamuzi wa katikati Florentina Zabron kutokea Dodoma ,Mwamuzi msaidizi namba moja Ferdinand Chacha wa Mwanza,mwamuzi msaidizi namba mbili Mashaka Mandemwa kutoka Mwanza,mwamuzi wa akiba Gelmina Simon wa Dar es Salaam na kamishna wa mechi anatoka Arusha,Peter Temu.
Wakati huo huo, droo ya Kombe la Shirikisho la Azam inafanyika kesho Ijumaa Machi 2, 2018 saa 5 asubuhi Makao Makuu ya Azam Tv wadhamini wa mashindano hayo.
Droo hiyo itahusisha timu nane(8) zilizofanikiwa kufuzu hatua hiyo ya Nane bora.
Timu zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo ni Young Africans na Azam FC za Dar es Salaam,Singida United ya Singida,Njombe Mji ya Njombe,Mtibwa Sugar ya Morogoro,Tanzania Prisons ya Mbeya,Stand United ya Shinyanga na JKT Tanzania ya Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...