Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
TUME ya Taifa ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS), inatarajia kuanza kampeni za kitaifa kuhamasisha wanaume kupima afya zao ,ili kujenga tabia ya kujitokeza kujua afya zao kwani ni asilimia 45 pekee ya kundi hilo walioaminika kuwa na VVU ndio waliopima kujua hali zao.
Aidha imeeleza ,kati ya watu kumi wenye maambukizi mapya kwa mwaka ,vijana wanne sawa na asilimia 40 ugundulika kupata maambukizi hayo.
Pamoja na hayo ,kati ya vijana kumi waliopata maambukizi mapya kila mwaka nane huwa vijana wa kike na wawili ni vijana wa kiume.Mkurugenzi mtendaji wa TACAIDS ,Leonard Maboko aliyaeleza hayo mjini Kibaha ,Mkoani Pwani ,katika mkutano ulioandaliwa na tume hiyo ,kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi mwamvuli ya mwaka 2018/2019 .
Alisema ,kampeni hiyo itakuwa ya miezi sita na itakuwa endelevu hadi hapo watakapohakikisha wanatokomeza ama kupunguza gonjwa hilo .Maboko alisema ,wale watakaobainika kuwa na maambukizi mapya watatakiwa kuanza tiba ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARVs) mapema ili kuondoa vifo vinavyotokana na virusi hivyo .
Alielezea ,wanaandaa kampeni hizo kutokana na takwimu za utafiti wa viashiria vya ukimwi ya mwaka 2016/2017 inayoonyesha idadi ya watu wanaopima na wanaogundulika kuambukizwa wanaoanza kutumia dawa ni wanawake kuliko wanaume.

Mratibu wa mtandao wa viongozi wa dini wanaoishi na virusi vya ukimwi ,(TANERELA),mchungaji Amin Sandewa pichani .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS ) ,Leonard Maboko akizungumza jambo ,mjini Kibaha ,Mkoani Pwani ,katika mkutano ulioandaliwa na tume hiyo ,kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi mwamvuli ya mwaka 2018/2019 .(picha na Mwamvua Mwinyi).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...