Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesema wizara yake itaifanyia mabadiliko makubwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kutokana na udhaifu mkubwa aliougundua kiutendaji, hali inayosababisha kutotimiza majukumu yake kwa ufanisi.

Naibu Waziri Aweso amesema kuwa tume hiyo kwa muda mrefu imekuwa haifanyi kazi yake vizuri na imembidi afike katika tume hiyo ili kufahamu undani wa tatizo hilo, kwa kuwa Serikali imeazimia kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji kwa lengo la kuhakikisha usalama wa chakula na kuunga juhudi za kuinua uchumi wa viwanda nchini.

‘‘Tuna zaidi ya hekta milioni 29.4 za ardhi kwa ajili ya kilimo, lakini hekta 468,000 sawa na asilimia 24 pekee ndio zimeendelezwa, hii manake bado tuko nyuma sana katika uzalishaji wa chakula pamoja na kuwa na eneo kubwa. Hili ni tatizo ambalo wizara italichukulia hatua za haraka’’, alisema Naibu Waziri.

Aliendelea kusema kuwa kuna haja ya kuipa nguvu sekta ya umwagiliaji kwa kuwa dhana ya uchumi wa viwanda inategemea sana kilimo cha umwagiliaji na sio kutegemea msimu wa mvua, ambacho kwa muda mrefu kimekuwa hakikidhi mahitaji ya taifa.

‘‘Sijaridhishwa kabisa na utendaji wa Tume ya Umwagiliaji na kuna tatizo katika menejimenti yenu na kusababisha utendaji mbovu, mabadiliko makubwa yanahitajika ili kuleta ufanisi wa tume hii ili tuanze kuona tija katika sekta ya umwagiliaji,’’ alisema Aweso.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Umwagiliaji, Mhandisi Seth Luswema amesema kuwa amefarijika na ujio wa Naibu Waziri kwa kuwa hawajawahi kuwa na kikao ambacho wameweza kueleza changamoto zao, na kukiri kuwa kuna kasoro nyingi za kurekebisha kiutendaji ili waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kikao kilichofanyika katika ofisi za tume hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mhandis Seth Luswema akitoa ripoti ya kuhusu sekta ya umwagiliaji kwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso katika kikao na watumishi wa tume hiyo.
Sehemu ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji waliohudhuria katika kikao na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...