Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda aliwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka, Mheshimiwa Maithripala SIRISENA.

Hii ni hatua muhimu katika kuendeleza, kuimarisha na kukuza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano mwema uliopo kati ya Tanzania na Sri Lanka ambao ulianza mnamo miaka ya tisini. Wakati huo, Sri Lanka ilikuwa inawakilishwa nchini Tanzania kupitia Ubalozi wake wa mjini Kampala, Uganda ambao baadaye ulifungwa na Tanzania ikiwakilishwa nchini Sri Lanka kupitia Ubalozi wake wa New Delhi. Kwa sasa Sri Lanka inakusudia kumteua Balozi wake mjini Nairobi ambaye pia ataiwakilisha nchi hiyo nchini Tanzania.

Katika hafla hiyo, Balozi Luvanda aliambatana na Mwambata Jeshi wa Tanzania nchini India, Col.Amri Salim MWAMI. Aidha, Balozi Luvanda alifanya mazungumzo na Mkuu wa Itifaki wa Sri Lanka pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Masuala ya Afrika, ambapo ameahidi kushirikiana kwa karibu na watendaji hao katika kudumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizi mbili na ambao utazinufaisha zaidi, hususan katika kuhakikisha uhaulishaji wa uzoefu, teknolojia na utaalam wa Sri Lanka kwa Tanzania kwenye sekta ya viwanda vya nguo, madini na vito mbali mbali na kilimo.

Sri Lanka ni nchi yenye uchumi unaoendelea ingawa imepitia kipindi kigumu cha vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa takriban miaka 25, vita ambavyo vilimalizika mwaka 2009.
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (kushoto) ambaye anawakilisha pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mheshimiwa Maithripala SIRISENA, Rais wa nchi hiyo
Balozi Luvanda akisalimiana na maafisa waandanizi wa Ikulu ya Sri Lanka
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda aliwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka, Mheshimiwa Maithripala SIRISENA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...