NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DODOMA
WAKATI kuna wimbi la uchomaji misitu ovyo hapa nchini, “Mtoto wa Mkulima, Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda ametoa “dawa” ya kuzuia uharibifu huo wa maliasili na si nyingine bali ni kufuga nyuki.
Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye alipenda kujitambulisha kama mtoto wa mkulima kutokana na mapenzi yake katika Kilimo, alitoa “elimu” hiyo leo Aprili 14, 2018 wakati akizindua nembo ya “Malkia wa Asali Tanzania” kwenye Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
“Sisi upande wa Katavi tulichofanya, nilmwambia mkuu wa Mkoa sisi kuchoma choama misitu ni “tradition” (utamaduni) yaani kuchoma ni jambo la kawaida na ukitaka kuzuia hili jaribu kutumia ufugaji wa nyuki kama silaha ya kuzuia uchomaji wa miti.” Alisema na kuendelea.
Kwa hivyo alichofanya maeneo kama Inyonga, tulitenga maeneo na kuweka mabango yetu tukaweka wafugaji wa nyuki na kuwaambia ninyi ndio walinzi wetu na tangu tufanye hivyo kumekuwepo na hali nzuri sana, na uchomaji moto umepungua sana, alisema.
Mheshimiwa Pinda alitoa mfano mwingine jijini Mbeya (Mbeya city), ambako mji umezungukwa na milima mizuri yenye misitu ambayo imekuwa ikiharibiwa na uchomaji moto mara kwa mara.
“Alitokea baba mmoja Askofu Mwalyego siku moja akaja kuniambia baba mimi hii inanikera kama inavyokukera sana wewe, hivi nikijaribu ku-introduce ufugaji wa nyuki hapa itasaidia, nikamwambia try (jaribu), ameweka wafugaji wa nyuki kuzunguka milima pale Mbeya mjini na mimi nikamwambia I will buy all your honey na juzi nikawa namuuliza zoezi langu linakwendaje, akaniambia nina miaka miwili mitatu sijaona moshi kwenye lile eneo.
Mhe. Pinda akiangalia Mvinyo (wine), uliotengenezwa na kampuni ya Nyuki safari ikiwa na nembo mpya ya Malkia wa Asali.
Mhe. Pinda akiungana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Kuandikwa, (wapili kulia), Mbunge wa Urambo, Mhe. Margareth Sitta, (wakwanza kushoto), Mwanzilishi mwenza na Afisa Mkuu Mbunifu wa kampuni ya kuzalisha asali ya Nyuki Safari, Mary Winzer Canning, (wanne kushoto), na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Profesa Silayo na mrembo aliyebeba nembo hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...