Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Viwanda, Biashara na Kilimo Tanzania (TCCIA) pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), wanautaarifu Umma kuwa wameandaa Mkutano wa Wadau utakaojadili na kupokea maoni kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi. 

Mkutano huu utawakutanisha Waajiri  na Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) wa Mikoa ya Dodoma na Singida; na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Eneo : Jengo la LAPF,
Mtaa wa Uhindini, Barabara ya Makole,
DODOMA.
Tarehe : 13 Aprili, 2018
Muda : 7:30 Mchana

Imetolewa na:

Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu,
Jengo la LAPF,
Mtaa wa Uhindini,
Barabara ya Makole,
S.L.P. 2890,


DODOMA, TANZANIA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...