Wagonjwa
467 wenye matatizo ya moyo wamebainishwa na kupatiwa huduma ya ushauri
na matibabu kutoka kwa madaktari bingwa waliotoa huduma kwenye kambi
maalumu ya siku 4 katika hospitali ya Vwawa-Mbozi Mkoani Songwe.
Timu
ya Madaktari Bingwa na wauguzi 5 wameeleza kuwa wagonjwa 18 kati ya hao
waliowahudumia wamepewa rufaa ya kufika hospitali za Rufaa kwa ajili ya
matibabu Zaidi.
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Moyo George Lyego Longopa Kutoka Taasisi ya
Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete amesema wameanza matibabu siku ya
Jumanne na kila Daktari amekuwa akiona zaidi ya wagonjwa 60 kutokana na
hamasa ya wagonjwa waliojitokeza kupata matibabu ya magonjwa ya moyo.
“Tumeona
wagonjwa wengi na tumeamini kuwa Songwe tatizo la Magonjwa ya moyo bado
ni kubwa, wagonjwa wengi wamekutwa na matatizo ya shinikizo la damu,
moyo kushindwa kufanya kazi vizuri pamoja na matatizo ya mishipa ya damu
kuziba”, amesema Dkt Longopa.
Afisa
Muuguzi Kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Flora Kasembe ameeleza
kuwa mtindo wa maisha ya wananchi wa Songwe unaweza kuwa ni chanzo cha
magonjwa ya moyo hasa kutokana na uwepo vyakula vingi lakini wananchi
hawali mlo kamili.
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Moyo George Lyego Longopa Kutoka Taasisi ya
Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete akichukua maelezo ya mgonjwa wa moyo
katika hospitali ya Vwawa-Mbozi.
Afisa
Muuguzi Kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Flora Kasembe akimpima
shiniko la damu mwandishi wa habari Manuel Kaminyoge katika hospitali
ya Vwawa-Mbozi,
Baadhi
ya wagonjwa wakisoma kipeperushi kinachoeleza masuala ya lishe wakati
wakisubiri kupata huduma ya madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Vwawa-Mbozi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...