Na
Mary Gwera
MAHAKAMA ya Tanzania imeingia
Mkataba na Shirika la Posta Tanzania kutoa huduma za usafirishaji wa nakala za
hukumu, barua na nyaraka muhimu za Mahakama.
Mkataba huo ulisainiwa
na Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta mapema
Aprili 05 katika Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mahakama ya Rufani-Dar es
Salaam.
Mkataba huu chini ya
huduma mpya ya Posta mlangoni (The post
at your doorstep) iliyoanzishwa na Shirika la Posta hivi karibuni, utalipa
jukumu la kukusanya na kusafirisha/kusambaza nakala za hukumu na nyaraka
mbalimbali za Mahakama na kuzifikisha kwa wahusika kulingana na anwani zao na
mahali walipo (Anwani za makazi).
Akizungumza kabla ya
utiani saini wa mkataba huo, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Bw. Hussein Kattanga
amesema kuwa hatua hii ni mwendelezo wa maboresho mbalimbali yanayoendelea
kufanyika ili kuwafikia wananchi.Aidha; Mtendaji Mkuu
amelitaka Shirika hilo kutekeleza makubaliano hayo kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja
na kusambaza nakala za hukumu na nyaraka nbyingine kwa wahusika na kwa wakati.
“Sitarajii kuona
wananchi wanapanga foleni Mahakamani kutafuta hukumu zao na nyaraka nyingine,
nina imani kuwa Posta mtafanya kazi ya kukusanya na kusambaza nyaraka hizo kwa
wananchi ipasavyo,” alisema Mtendaji Mkuu.Naye Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe.
Katarina Revocati ameeleza kufurahishwa kwake na utiaji saini wa Mkataba huo
kwani utasaidia kufikia ndoto ya Mahakama ya muda mrefu ya kuwafikia wananchi
kwa karibu zaidi.
“Naomba kusema kuwa,
nimefurahishwa sana na hatua hii , kwani ni ndoto ya Mahakama ya muda mrefu,
vilevile hatua hii itarahisisha utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Jaji Mkuu ya
kutoa nakala za hukumu bure kwa zitawafikia wananchi popote watakapokuwa,”
alisema Mhe. Revocati.Kwa upande wake Posta
Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Hassan Mwang’ombe alisema
alimuhakikishia Mtendaji Mkuu wa Mahakama kuwa watafanya kazi hiyo kwa ufanisi
mkubwa.
“Kusainiwa kwa Mkataba
huu kutawezesha pia kuongeza kasi ya usambazaji wa barua za kawaida za Mahakama
kuwafikia walengwa mapema zaidi kwani zitachukuliwa Mahakamani na Maofisa wa Posta na kupelekwa
moja kwa moja kwa wahusika/mhusika,” alisema Bw. Mwang’ombe.
Vilevile Mkuu huyo
alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Maofisa wa Posta hususani kwa
kuandika anwani za makazi pamoja na postikodi.
Hafla hiyo fupi
ilihudhuriwa na baadhi ya Maafisa Waandamizi kutoka Mahakama ya Tanzania pamoja
na Shirika la Posta Tanzania.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe, akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Posta na Mahakama ya Tanzania wa huduma ya Posta Mlangoni inayotolewa na shirika hilo. Hafla hiyo, imefanyika katika Ofisi za Mahakama ya Rufani, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa TPC, Zuhura Pinde. Waliosimama nyuma yao, ni baadhi ya Maofisa waandamizi wa Posta na Mahakama.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia), akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga. Wengine nyuma kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Fadya Zam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPC, Elia Madulesi, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Solanus Nyimbi.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia), akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga. Wengine nyuma kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Fadya Zam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPC, Elia Madulesi, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Solanus Nyimbi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...