Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amkutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza  Mhe. Penny Mordaunt .
Makamu wa Rais ambaye amewasili nchini Uingereza leo kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Katika mkutano wake na Waziri huyo wa Uingereza Makamu wa Rais alielezea hatua kubwa iliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika Elimu mara baada ya kuamua Elimu iwe bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.
Pia Makamu wa Rais alishukuru mradi wa DFID unatekelezwa mkani Simiyu na kuomba mradi huo uongezewe maeneo ili uweze kuwanufanisha watoto wengi wa kike.
Makamu wa Rais pia alizungumzia namna Majukwaa ya Kuwawezesha wanawake kiuchumi yanavyofanya kazi huku taratibu mbali mbali zinafanyika ili mabenki yaweze toa mikopo kwa riba nafuu.
Mwisho Makamu wa Rais alizungumzia jitihada mbali mbali zinazofanywa na Serikali katika kuboresha Mazingira ya kufanya Biashara nchini.
Naye Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada wanazofanya katika kuboresha huduma za kijamii, alisema nchi yake ipo tayari kusaidia katika masuala ya makusanyo ya kodi, kuboresha uwezo wa walimu kwa kuwapatia mafunzo mbali mbali.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt jijini London. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt(kushoto) jijini London. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Agustine Mahige jijini London. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akipokelewa na  Balozi wa Tanzania Nchi Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro alipowasili jijini London.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mbele ya Balozi wa Tanzania Nchi Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro jijini London. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...