Hospitali ya Taaluma na Tiba ya
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, MAMC iliyopo Mloganzila
imefanya warsha ya mafunzo ya maadili ya taaluma kwa wanafunzi wa
shahada ya uzamili.
Akizungumza katika warsha hii Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Huduma za Hospitali, Prof. Said Aboud amesema msingi wa huduma zinazotolewa na hospitali ya Taaluma na Tiba, MAMC umemlenga mgonjwa na hivyo kiwango cha hali ya juu cha maadili ya taaluma kinahitakiwa ili tuweze kufikia lengo hili.

Prof.
Aboud amesisitiza kuwa wanafunzi wa shahada ya uzamili katika fani za
afya ambao tayari ni madaktari, wafamasia, wauguzi n.k ni nguvu kazi
muhimu sana katika hospitali kwa hiyo ni muhimu kuhakikisha wanatoa
huduma nzuri kwa wateja ambao ni wagonjwa na pia kuzingatia kutoa
taarifa zilizo sahihi na kwa wakati kwa mgonjwa au ndugu wa mgonjwa.
Naye Mkurugenzi wa Mafunzo ya Uzamili, Dkt Emmanuel Balandya amekumbusha kuwa MUHAS inazingatia masuala ya maadili ya kitaaluma kwa umakini sana na ndio maana yamesisitizwa wakati walipoanza mafunzo na kufundishwa katika muhula wa kwanza wa masoma.

Na
kwa kuwa mafunzo haya ni endelevu, Dkt Balandya ameeleza, imeonekana ni
muhimu kuwa na warsha hii katika kipindi hichi cha mpito kutoka masomo
ya sayansi za msingi (basic sciences) kwenda kwenye masomo ya sayansi za
kliniki (clinical sciences). Dkt. Balandya amewasisitizia kuwa
washiriki wa warsha hii kuwa namna wanavyomjali mgonjwa ni muhimu zaidi
kuliko kile wanachokijua.
"Tunaweza kushindwa kuhakikisha kuwa wagonjwa wote wanapona lakini tunaweza kubadilisha maisha yao kwa namna tunavyowahudumia kwa kuwajali", aliongeza. Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba MAMC, Dkt Hendry Sawe amesema warsha hii ya maadili ya kitaaluma kwa watu wa fani za afya (madaktari, wafamasia, wauguzi n.k) imelenga namna ya kufanya kazi kitaaluma kwa kuzingatia kanuni za ufanyaji kazi za taaluma husika.

Hii
ni muhimu kwa sababu watoa huduma wa afya wanahusika moja kwa moja na
maisha ya watu (wagonjwa). "Mafunzo haya yamejikita kwa wanafunzi wa
shahada ya uzamili kwa sababu wengi wao ni viongozi wajao katika fani
mbalimbali za afya nchini", aliongeza Dkt Sawe.

Kutoka kulia, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, MAMC, Dkt Hendry Sawe, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Huduma za Hospitali, Prof. Said Aboud, Mkurugenzi wa mafunzo ya Uzamili, Dkt Emmanuel Balandya na Mkurugenzi wa Mafunzo Endelevu na Maendeleo ya Uweledi Dkt Doreen Mloka wakifuatilia ufunguzi wa warsha ya maadili ya kitaaluma kwa wanafunzi wa shahada ya uzamili wa afya, MAMC.

Mratibu wa warsha ya maadili ya kitaaluma ya wanafunzi wa shahada ya uzamili wa fani za afya, Dkt Francis Furia akiongoza kipindi majadiliano wakati wa warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano MAMC

Mwanafunzi wa shahada ya uzamili, MUHAS akichangia hoja wakati wa kipindi cha majadiliano katika warsha ya maadili ya kitaaluma kwa wanafunzi wa shahada ya uzamili wa afya ilitolewa na hospitali ya taaluma na tiba, MAMC iliyopo Mloganzila
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...