
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt.
Susan Kolimba na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA)
Mhe. Martin Ngoga wakisalimiana walipokutana kwa mazumgumzo katika Ofisi
za Wizara Dodoma.
Mhe.
Ngoga alimtembelea Naibu Waziri Mhe. Dkt. Kolimba Ofisini kwake ambapo
walifanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Jumuiya. Mhe.
Dkt.Kolimba katika mazungumzo hayo amemwahidi Spika wa EALA kuwa Wizara
na Serikali kwa ujumla itatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Bunge hilo
katika utelezaji wa majukumu yake.
Aidha
kwa upande wake Spika wa EALA amesema kuwa,kwa sasa wamejipanga vizuri
katika kuhakikisha wanadumisha ushirikiano na Mabunge ya Nchi wanachama
na kutoa mrejesho kwa Nchi wanachama kuhusu masuala mbalimbali ya
yanayojili katika Bunge hilo.
Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linafanya vikao vyake mjini Dodoma kuanzia tarehe 9 hadi 28 Aprili, 2018

Spika
wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Mhe. Martin Ngoga
akisaini kitabu cha wageni mara baada kuwasili Wizarani Dodoma.

Naibu
Waziri Mhe. Dkt. Kolimba na Spika wa EALA Mhe. Dkt.Ngoga wakiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya Wabunge wa EALA na Maafisa kutoka Wizarani
na Bunge la EALA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...