Zaidi ya watu 20 wanadaiwa kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia ajari ya basi la kampuni ya City bus lililogana uso kwa uso na fuso katika kijiji cha makomelo wilayani Nzega mkoani TABORA.
Ajari hiyo imetokea usiku wa kuamkia Leo katika kijiji hicho baada ya kudaiwa dereva wa fuso kutaka kukwepa shimo na kujikuta fuso hilo likimshinda,hivyo kupelekea kugongana USO kwa USO.
MPAKA sasa kamanda wa jeshi la polisi mkoani TABORA na viongozi wengine wa serikali wamefika katika eneo la tukio huku basi hilo likitarajiwa kunyanyuriwa ili kuona kama kuna watu wengine waliosalia.
Hata hivyo miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospital ya wilaya ya Igunga kwa ajili taratibu zingine.
Globu ya Jamii inafuatilia kwa ukaribu tukio hili,itaendelea kuwaletea taarifa kadiri ya zitakavyokuwa zikipatikana kutoka Mamlaka husika.
Mungu azilaze roho za Marehemu mahali pema peponi-Amen



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...