Na Munir Shemweta, Morogoro

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi amesisitiza umuhimu wa kuwashirikisha watumishi katika mipango ya uendeshaji Taasisi kwa kuwa suala hilo lipo kisheria.

Aidha, alisema kwa miaka yote Serikali imekuwa ikisisitiza Taasisi kujenga na kutekeleza utaratibu wa kushirikisha watumishi na hali hiyo inatokana na ukweli kuwa palipo na watumishi wengi pana mawazo mengi.Profesa Kabudi alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifungua mkutano wa kumi na tatu wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro.

‘’Ushirikishwaji watumishi kwenye mipango ya uendeshaji ofisi unasaidia kupata mawazo mengi na mapya yanayoweza kurahisisha uendeshaji wa ofisi na kutoa fursa ya kusikiliza kero na changamoto kwenye uendeshaji wa Taasisi na kushirikiana katika kutafuta ufumbuzi’’ alisema profesa Kabudi.

Aliongeza kuwa, kwa kushirikiana na watumishi ni dhahiri wanapata morari wa kushiriki kikamilifu kwenye utekelezaji wa mipango ya taasisi ambayo wao wenyewe walishiriki kuiandaa.Waziri huyo wa Katiba na Sheria alisema, ushirikishwaji unafanywa kupitia baraza la wafanyakazi kwa kuwa baraza ni chombo kinachowashirikisha wafanyakazi katika kupanga , kusimamia na kutekeleza mipango mbalimbali inayohusu shughuli za kazi za Taasisi kama zilivyoainishwa katika sheria za nchi.
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume Casmir Kyuki na kulia ni Katibu wa Baraza Ambokile Mwakasungula (Picha na Munir Shemweta-TUMESHERIA)
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Casmir Kyuki (Kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro, kulia ni Katibu wa Baraza Ambokile Mwakasungula (Picha na Munir Shemweta-TUMESHERIA)
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akimsikiliza Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Khalist Luanda mara baada ya kufunguka mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Tume ya Kurekebisha Sheria uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro, katikati ni Katibu Msaidizi wa Tume (Idara ya Mapitio) Angelah Bahati (Picha na Munir Shemweta-TUMESHERIA)
Sehemu ya Wajumbe Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano huo uliofanyika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...