Na
Sixmund J. Begashe
Rais
wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) Bw Adrian Nyangamale
ameungana na wasanii wote, wapenda sanaa, Serikali ya Tanzani, na watanzania
wote katika kuomboleza kifo cha aliewahi kuwa Kahimu Mkurugenzi wa Idara ya
Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni nchini Bi Joyce Hagu.
“Nimepokea
kwa mshtuko na masikitiko makubwa msiba wa Dada Joyce Hagu, ni juzi tu
tulikuwanae Magomeni kwenye msafara wa Mh Waziri Dr Harison Mwakyembe
alipotembelea wanamuziki wa zamani, tukitaniana na kucheka kama ilivyokuwa desturi
yake, kumbe ndio alikuja kutuaga.’’ Aliandika Bw Nyangamale kwenye kundi la
whatsap la shirikisho hilo lijulikanalo kama JAMVI.
Kupitia
ukurasa huo maarufu nchini wa JAMVI Bw Nyangamale aliongeza kuwa Marehemu Joyce Hagu alikuwa msaada mkubwa
kwenye tasnia ya sanaa za Ufundi nchini kwa kutumia taaluma yake ya sanaa
kuuwashauri wasani mambo muhimu katika Sanaa na Utamaduni wa Mtanzania, kukosa
na kutoa njia bora ya kujisahihisha pale wasanii wanapo kwende kinyume na
maadili ya Utamaduni wa Mtanzania.
“Shirikisho
la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) tunatoa pole kwa Mhe Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, watumishi na wafanyakazi wa Wizara, na Taasisi
zake, Mashirikisho ya Sanaa, Vyama, Vikundi na Jamii yote ya wasanii nchini.
Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote bila kusahau Wanajamvi
kwa msiba huu mzito.” Alimalizia Bw Nyangamale
Wakiungana
na Rais wa TAFCA, wanajamvi Lilian Nabora, Mussa Sango, Wilhadi Tairo na
Namsikiliza Mungu wameeleza kwa masikitiko makubwa namna walivyo pokea taarifa
za msiba huo na kuwa Marehemu amefariki wataki ikiwa bado machango wake ulikuwa
ukihitajika sana katika tasnia ya Sanaa na Utamaduni nchini, na kuahidi kuwa
wataendelea kumkumbuka daima.
Taarifa
za kuaga dunia kwa Msanii Msomi na Mwalimu gwiji wa sanaa nchini Bi Joyce Hugu zimedhibitishwa
na kaka yake aitwae Gabriel pale alipo ongea kwa simu na mwandishi wa habari
hizi akisema kuwa dada yao amekutwa na umauti akiwa amelala usiku wakumakia
jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...