Na Agness Francis,Blogu ya Jamii
MECHI ya wana Paluhengo Lipuli na vinara wa Ligi Simba uliotarajiwa kuchezwa Ijumaa Aprili 20 mwaka huu katika Uwanja wa Samora Mjini Iringa imesogezwa mbele.
Mchezo huo wenye namba 202 wa Ligi Kuu ya Vodacom Lipuli dhidi ya Simba SC sasa hautachezwa kama tarehe ya mwanzo iliyopangwa na (TFF).Umesogezwa mbele kwa siku moja.
Bodi ya Ligi ya Mpira wa miguu Tanzania (TFF) wameamua Mechi hiyo ichezwe Aprili 21,mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Samora mkoani Iringa.
Ambapo Sababu za mabadiliko hayo ni wamiliki wa uwanja kuutumia Aprili 20, 2018 kwa shughuli nyingine za kijamii.
Ikiwa kwa mujibu wa ratiba Mbeya City inasubiri kuvaana na Yanga SC Aprili 22 mara baada ya kurejea.
Kikosi hicho ambacho kipo nchini Ethiopia kuchuana na Welaita Dicha Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Mtanange huo utakaopigwa katika Dimba la Uwanja wa Sokoine uliopo Jijini Mbeya huku Mbeya city wakiwa wenyeji wa Yanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...