Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MVUA zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam zimeendelea kuleta madhara katika maeneo ya Mikocheni barabara ya Chato mtaa wa Lukuledi baada ya barabara hiyo kukatika na kujaa maji.
Akizungumza na Michuzi Blog, Kaimu Meneja uhusiano wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam(DAWASCO) Everlasting Lyaro ameeleza maji hayo ni ya mvua na karavati linalomwaga maji hayo ni yale yanayokusanywa maeneo ya Mwenge, Mwananyamala na Mikocheni.
Aidha ameeleza walienda eneo la tukio na kugundua tatizo hilo halikuwa lao bali ni watu wa ujenzi wa barabara chini ya Manispaa na tayari suala hilo limekabidhiwa kwa makandarasi waliojenga barabara hiyo.
Pia ametoa rai kwa wananchi kwa kuwataka kuhifadhi miundombinu hasa mita zitakazosombwa na maji na watakaokumbwa na tatizo hilo watarekebishiwa mita hizo bure. Amewataka wananchi kutoa taarifa kwa maeneo yatakayokosa huduma ili washughulikie mara moja.
Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo Abdul Rashid ameeleza tukio hilo lilianza jana saa nane mchana baada ya magari kadhaa kupita ghafla barabara ilishuka na maji kuanza kumwagika hali iliyosababisha barabara kushindwa kupitika na ugumu wa biashara.
Hadi waandishi wetu wanaondoka eneo la tukio sehemu ya barabara hiyo iliendelea kukatika.
Muonekano wa mtaa wa Lukuledi barabara ya Chato baada ya kukatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam.
Mpita njia akijaribu kukwepa shimo lililopo katika barabara ya Chato, Mikocheni jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Muonekano wa mtaa wa Lukuledi barabara ya Chato baada ya kukatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam.
Mpita njia akijaribu kukwepa shimo lililopo katika barabara ya Chato, Mikocheni jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...